Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) – ABNA – Sherehe ya bulugh kwa wasichana imefanyika kwa adhama katika mji mtakatifu wa Karbala, Iraq. Takribani wasichana 5,000 kutoka shule 121 walishiriki kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na Ataba ya Abbasiyya. Tukio hilo lililenga kuwapa wasichana hawa utambuzi wa kidini na kuadhimisha hatua muhimu ya kuingia katika umri wa kuwajibika kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Sherehe hiyo imekuwa tukio lenye mvuto mkubwa, likiambatana na hotuba, mawaidha na maombi, na kuwapa washiriki fursa ya kuimarisha uhusiano wao na mafundisho ya AhlulBayt (a.s).
22 Aprili 2025 - 18:16
News ID: 1551438
Your Comment